Isaiah 7:11-14

11 a“Mwombe Bwana Mwenyezi Mungu wako ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana.”

12 bLakini Ahazi akasema, “Sitaomba; sitamjaribu Bwana.”

13 cNdipo Isaya akasema, “Sikia sasa, ewe nyumba ya Daudi! Je, haitoshi kujaribu uvumilivu wa wanadamu? Je, mtaujaribu uvumilivu wa Mungu wangu pia? 14 dKwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli.
Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi.
Copyright information for SwhKC